London, England. Bastian Schweinsteiger (32) amepanga kuondoka Manchester United ili kutua Chigago Fire kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mchezaji huyo wa Manchester United na nahodha wa zamani wa Ujerumani, anatarajia kujiunga na Chicago Fire mwishoni mwa msimu huu.
Schweinsteiger ameripotiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja akiwa ni mchezaji wa kwanza kutoka Old Trafford kuonyesha njia ya kutimka.
Mchezaji huyo amesaini klabuni hapo ilipokuwa chini ya kocha aliyepita, Lous van Gaal mwaka 2015. Hata hivyo, tangu aingie Jose Mourinho klabuni hapo, amejikuta akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Mchezaji huyo mwenye miaka 32 amefunga bao moja na kucheza michezo minne.
0 comments:
Post a Comment