Social

Monday, April 10, 2017

Wasomi, wanasiasa ‘wampa 5’ Nape


 Mbunge wa  Mtama, Nape Nnauye ameungwa mkono na wanasiasa na wasomi mbalimbali kwa ushauri wake kwa kumtaka Rais John Magufuli kuunda tume kuchunguza vitendo vya utekaji vinavyoendelea nchini.
Nape alitoa ushauri huo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye jimbo lake, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoachwa kwenye baraza la mawaziri, mwezi uliopita.
Katika mkutano huo, Nape alisema iwapo Rais Magufuli hataunda tume kuchunguza matukio ya utekaji na uvamizi, wananchi watajenga chuki dhidi yake wakidhani ndiye anayewatuma.
 Wakizungumzia kauli za mwanasiasa huyo, baadhi ya wanasiasa na wasomi walisema Nape ana nia njema na Rais Magufuli, ndiyo maana amejitokeza kumshauri kuhusu mambo ambayo yanawakera wananchi.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema kuna haja Rais Magufuli akaunda tume kama alivyopendekeza ili ijulikane wazi kama matukio ya utekaji ni ya kijinai au ni ya kisiasa. Pia, watu walio nyuma ya matukio hayo wafahamike na kuchukuliwa hatua.
Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara alisema Nape ni mtu ambaye amekulia ndani ya CCM, anakijua vizuri chama hicho, kwa hiyo anachokisema anakijua na kina ukweli kwa sababu kila Mtanzania anakiona.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi alisema anachokisema Nape ndicho kilichopo kwenye vichwa vya watu mbalimbali kwa sasa bila kuangalia itikadi zao za kisiasa.

0 comments:

Post a Comment