Vitendo vya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha, kufuata na polisi wenye silaha wanapokwenda kudai kodi kwa wafanyabiashara, vimemshtua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kupiga marufuku tabia hiyo.
"Kuna watu wachache ambao wanataka kuifanya Serikali ionekane haina mwelekeo, tunawafuatilia tukiwagundua tutawatoa sadaka," alisema Gambo.
Gambo aliyasema hayo kwenye mkutano uliowashirikisha wafanyabiashara, watendaji wa Serikali na maofisa wa TRA mwishoni mwa wiki iliyopita na kwamba, siyo busara kukusanywa kodi kwa vitisho.
Alisema kwa sasa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kuwa na hofu na kufikiria kutowekeza kutokana na matukio ya watu wachache, ambao wanataka kuiyumbisha Serikali.
Awali, baadhi ya wafanyabiashara walilalamikia utaratibu wa ukusanyaji kodi wakisema unafanywa bila kuzingatia sheria.
0 comments:
Post a Comment