
Mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi CUF umepiga hatua nyingine baada ya viongozi wawili wakuu, mwenyekiti Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu, Seif Sharif, kutoa hadharani kauli zinazokinzana.
Lipumba akizungumza na chombo kimoja cha habari ametofautiana na Maalim Seif akisema ni afadhali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kuliko Maalim Seif aliyejitangazia matokeo. Anasema Seif alifanya kosa kubwa kujitangazia matokeo. DW imezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Tanzania Bwana Hussein Sengu kuhusu hali hiyo ya vuta nikuvute katika chama.
0 comments:
Post a Comment