
Juba, Sudan Kusini. Rais Salva Kiir amemfukuza kazi mara moja mkuu wa Jeshi, Jenerali Paul Malong na hadi jana ilikuwa haijatolewa sababu kuhusu uamuzi huo.
Ingawa hakuna sababu yoyote iliyotolewa, katika siku za hivi karibuni maofisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu. Jenerali Malong anaonekana na Wasudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo.
Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo vimeiingiza Sudan Kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.
0 comments:
Post a Comment