Wachezaji wa Bayern Munich, Arjen Robben na Frank Ribery licha ya kuongezewa mkataba hadi mwaka 2018, imeelezwa kwamba viwango vyao vimeporomoka msimu huu.
Kiungo wa zamani wa timu hiyo, Dietmar Hamann alisema wachezaji hao wanaonekana kupotea msimu huu kutokana na kushindwa kuonyesha makali yao.
Alisema kwamba ni vyema klabu hiyo ikafikiria kusajili vijana ambao wataitumikia timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.
ôWachezaji hao umri wao ni mkubwa, Bayern inatakiwa kufikiria upya kuhusu jambo hilo. Itafute wachezaji wanaokwenda na mfumo wa soka la kisasa na walio kwenye kiwango cha juu, bila shaka Alexis Sanchez anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji vijana ambao ni chaguo la kocha
0 comments:
Post a Comment