Cristiano Ronaldo anategemea kufikia Lionel Messi kwa kutwaa tuzo ya tano ya Ballon dÆOr mwaka huu.
Hiyo ni baada ya nyota huyo wa Real Madrid kuwekwa katika ukurasa wa mbele wa jarida la France Football, linalotoa tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa mwaka.
Gazeti hilo katika picha hiyo liliweka swali: ôNani wa kumshinda huyu kwa sasa?ö
Ronaldo(32), ambaye alitwaa tuzo yake ya nne mwaka jana baada ya kufunga penalti iliyopa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa na kuiongoza Ureno kutwaa ubingwa wa Euro 2016.
Tuzo hiyo ilimfanya kuwa nyuma kwa tuzo moja kwa mpinzani wake nyota wa Barcelona.
Ronaldo amejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa tuzo hiyo endapo ataiongoza Real kutetea ubingwa wake wa Ligi ya Mabingwa pamoja na kutwaa ubingwa wa La Liga.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amefunga mabao matatu katika nusu fainali dhidi ya majirani zao Atletico wiki iliyopita na tayari amefunga mabao matano dhidi ya Bayern katika robo fainali.
Kiwango hicho ndicho kilichomfanya apewe nafasi ya kushinda tuzo hiyo ya Desemba wakati gazeti hilo la Ufaransa lilipoandika: ôWakati mbio zikielekea mwishoni? Siyo lazima sana, lakini CR7 anakaribia kufikia hapo.
Kumfikia alipo, kunahitaji kuonyesha kitu cha zaida zaidi na kwa haraka.ö
Wengine wanaowania tuzo hiyo mbali ya Messi ambaye ameshindwa kuingia katika orodha ya nne bora.
Kipa wa Juventus, Gigi Buffon ndiye anayeonekana ni mshindani wa kweli wa Ronaldo, wengine ni mshambuliaji wa Atletico, Antoine Griezmann na chipukizi wa Monaco, Kylian Mbappe.
France Football liliongeza: ôMessi hajacheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa pili mfululizo.
0 comments:
Post a Comment