Social

Thursday, May 11, 2017

Nape, Kitwanga wapaza sauti


Dodoma. Kilio cha kutaka maji safi kilichosikika nchi nzima wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kilijiwa kwa ahadi kemkem na jana kilipazwa na wabunge baada ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuomba Sh672.2 bilioni ambao zimeonekana kuwa ni ndogo.
Mjadala mkali uliibuka jana baada ya Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge kusoma hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18 inayoonyesha Sh623.6 bilioni zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo.
Miongoni mwa watu waliozungumza kwa hisia kali kupinga bajeti hiyo, ni waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya John Magufuli, Charles Kitwanga (Mambo ya Ndani) na Nape Nnauye (Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa).
Fedha hizo ni chini ya kiwango cha mwaka wa fedha unaoisha ambao wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge Sh939.6 bilioni, kati ya hizo Sh915.1 bilioni zilitengwa kwa ajili ya maendeleo.
Hata hivyo, hadi Machi ni Sh184.1 bilioni sawa na asilimia 19.8 tu ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge  ndizo zilipelekwa wizarani.
"Rais John Magufuli alikuja bungeni na kuahidi kuwatua ndoo vichwani wakinamama, jambo ambalo ni tatizo kubwa," alisema Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe.
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga alikwenda mbali zaidi na kutuhumu kuwa Serikali haipeleki maji kwenye vijiji vyake kwa sababu inamuandaa mtu aliyemtaja kwa jina la Bashite kugombea ubunge kwenye uchaguzi  ujao.
Kitwanga alikuwa akifikisha kilio cha maji katika Kijiji cha Kolomijee wilayani Misungwi mkoani Mwanza, ambako Bashite alizaliwa.
"Sasa safari hii patachimbika. Na mimi sitatoa shilingi, nitakachofanya nitakwenda kumobilize (kuhamasisha) wananchi wa Misungwi kama 10,000 tukazime ule mtambo," alisema.

0 comments:

Post a Comment