Social

Wednesday, April 12, 2017

Rais Magufuli awasili kwenye uzinduzi wa reli ya Pugu


Dar es Salaam. Rais John Magufuli  ameshafika katika eneo la Pugu  nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya Standard Gauge itakayotumia umeme.
Ujenzi huo unaashiria kuingia hatua ya pili ya ujenzi baada ya ile  ya awali ambapo mkataba wa. ujenzi ulitiwa saini na kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchin Rahco na kampuni wabia wa zabuni ambao ni kampuni ya  Merkez ya Uturuk na Mota-Engil ya Ureno Februari 3 mwaka huu.
Gharama za ujenzi huu awamu ya kwanza kati ya DSM mpaka Morogoro itagharimu shilingi Trilion 2.7.

0 comments:

Post a Comment