
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kesho itaanza kutoa huduma mpya na ya kisasa ya upasuaji kwa njia ya matundu madogo kwa wanawake wenye tatizo la uvimbe kwenye mirija na mfuko wa uzazi.
Kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na mafunzo ya upasuaji kwa vitendo yanayotumia kwa hadubini ambayo madaktari wameanza kupewa jana na wataalamu mbalimbali Hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi leo katika warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama Vincent Tarimo amesema idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye mirija ya uzazi imeongezeka kwa kasi nchini na pia amesisitiza kwamba hospitali ya taifa sasa itaanza kutoa huduma ya matibabu kwa wanawake wenye matatizo hayo kwa gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment