Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, amefunguliwa mashtaka ya uhaini, kwa mujibu wa mkuu wa polisi nchini humo.
Alikamatwa kufuatia madai kuwa msafara wake ulikataa kuupisha ule wa rais Edgar Lungu.
"Imebainika kuwa kiongozi huyo wa upinzani alipuuza maagizo ya polisi ya kuondokea msafara wa raisi, na hivyo kuyaweka maisha ya rais hatarini, mkuu wa polisi Kakoma Kanganja, aliliambia shirika la Reuters.
Alikamatwa siku ya Jumatatu usiku baada ya polisi kuvamia nyumba yake mjini Lusaka.
Mkewe amekiambia kituo cha runinga cha nchi hiyo Muvi TV kuwa polisi walitaka kumuua mumewe.
0 comments:
Post a Comment