Social

Thursday, April 13, 2017

Viongozi wamtaka Lipumba kung’oka


Dar es Salaam. Licha ya Profesa Ibrahim Lipumba kuendelea na uenyekiti akifanyia shughuli zake ofisi ya makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam, baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuandika barua ya kumtambua,  viongozi wa matawi zaidi ya 50 ya chama hicho yamemtaka kung'oka.
Msimamo huo ulitolewa jana na viongozi walipozungumza na waandishi wa habari jana katika Hoteli ya Vina iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao walisema iwapo Profesa Lipumba atakaidi, watalazimika kutumia nguvu, bila aina ya nguvu hizo.
 Upande unaompinga Lipumba unaongozwa na Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na unaendesha shughuli zake makao makuu ya chama hicho yaliyopo Mtendeni, Zanzibar.
Hata hivyo, Magdalena Sakaya ambaye ameteuliwa na Profesa Lipumba kukaimu nafasi ya katibu mkuu, alisema watu hao ni kikundi cha wanachama wachache wanaotumiwa.

0 comments:

Post a Comment