Social

Wednesday, April 5, 2017

Sumaye aihakikishia ushindi Chadema


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye  pia ni


Geita. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye  pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema uchaguzi mkuu ujao Chadema itashinda kwani CCM imepoteza mwelekeo kuanzia kwa wanachama na viongozi kutokana na Serikali kuahidi kuwainua wanyonge, lakini wamezidi kuwa maskini.
"WanaCCM wamechoka kwa sasa wapo kwenye hofu kubwa wanatamani kuondoka hata leo, lakini wanajua wakiondoka hali yao itakuwa mbaya zaidi hakuna viwanda walivyoahidi wananchi maisha yamekuwa mabaya zaidi," alisema Sumaye.
Aliyasema hayo kwenye kongamano la Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Geita lililofanyika juzi mjini hapa.
Kuhusu mchakato wa katiba, Sumaye alisema Serikali ilitumia fedha za walipa kodi kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, lakini yamefungiwa kabatini baada ya  Rais John Magufuli kudai hakuwaahidi Watanzania Katiba Mpya wakati wa kampeni.
Alisema Rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato huo akiwa Mwenyekiti wa CCM na sasa chama hicho kina mwenyekiti mpya, lakini kinashindwa kumuagiza aendeleze mchakato huo waliouanzisha.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, Ansbert Ngurumo alisema chama hicho kinawategemea vijana kuleta mabadiliko na kuwataka kutumia mitandao ya  jamii kutafuta maarifa zaidi.

0 comments:

Post a Comment