Social

Friday, April 7, 2017

Malori, madereva washikiliwa Zambia


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), Angelina Ngalula amesema malori 200, madereva na wafanyakazi zaidi ya 400 wamekamatwa na polisi nchini Zambia.
Malori hayo yenye magogo yaliyokuwa yakisafirishwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuja Tanzania, yameshikiliwa nchini humo.
Kushikiliwa kwa malori hayo pamoja na madereva kunatokana na magogo yaliyobebwa, kuvunwa kwenye misitu ya nchi hiyo.
Alipopigiwa simu, Msemaji wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga alisema hana taarifa hizo na akataka apigiwe Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Alipopigiwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma, simu yake ilipokewa na mmoja wa maofisa ambaye alisema kuna malori ya Watanzania yanayoshikiliwa nchini humo.

0 comments:

Post a Comment